Ña Angela Msimbira OR-TAMISEMI Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watuwenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha zinawatambua na kuendelea kutoa mikopo ya Vijana kupitia Mikopo ya asilimia kumi ili kuendeleza juhudi zilizoonyeshwa na wadau wa Maendeleo nchini.Amesema hayo Julai 27,2022 Jijini Dodoma
Ña Angela Msimbira OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watuwenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha zinawatambua na kuendelea kutoa mikopo ya Vijana kupitia Mikopo ya asilimia kumi ili kuendeleza juhudi zilizoonyeshwa na wadau wa Maendeleo nchini.
Amesema hayo Julai 27,2022 Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa wakati akifunga rasmi program ya Feed the Future Tanzania inua vijana chini Tanzania chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani,USAID Tanzania.
Prof Ndakichako amesema kuwa vijana ni nguzo na rasilimali muhimu katika Taifa hivyo Serikali imekuwa ikuchukua hatua za kuhakikisha kwamba inaleta ustawi kwa vijana na kuweka Mazingira wezeshi ya kuweza kupata maendeleo, hivyo kila Halmashauri inawajibu wa kutenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana kichumi kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu.
Prof. Ndalichako ameiagiza Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kuhakikisha Vijana wanaedelea kuwezeshwa kwa kujengewe uwezo na kupewa vitendea kazi ili waweze kujikwamu kiuchumi Na kuleta maendeleo nchini.
Aidha, Prof. Ndalichako amezitaka Wizara na Taasisi zote zinazohusiana na ustawi wa jamii kushirikiana kwa pamoja kwa kuweka Mpango Mkakati wa kushughulika changamoto zinazoakabili vijana wa makundi yote nchini.
Akiongea kwa Niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mkurugenzi wa utawala kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI Victor Kategere amelishukuru shirika la Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani,USAID Tanzania kwa kuwainua vijana kiuchumi na kuwapongeza Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zilizonufaika na mradi huo kwa usimamizi uliotukuka.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la USAID, Kate Somvongisiri amesema Programu hiyo imehusisha vijana wa vijijini wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 kujihusisha na biashara ya kilimo na minyororo mingine ya thamani na kuongeza fursa zao za kiuchumi huku wakikuza uongozi na maisha bora.
” Tunajivunia kuwa mradi huu Inua Vijana umewafikia zaidi ya vijana 43,000 na kutoa zaidi ya shilingi bilioni 5.3 (dola za Marekani milioni 2.3) kama ruzuku kwa biashara na kilimo zinazomilikiwa na vijana.”amesema Somvongisiri.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Rashid Chuachua amesema kwa Mkoa wa Mbeya, vijana 14,000 wamenufaika na kati ya hao vijana 1,000 wamefikia mafunzo ya uongozi, vijana 3,000 wamepata mafunzo ya ujasiliamali na takribani vijana 10,000 wamefikia na mafunzo ya stadi za maisha.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amewataka vijana walionufaika na programu ya Feed the Future kutumia mafunzo hayo kuzalisha na kupiga hatua na kuleta faida kwa jamii inayowazunguka.
Aidha, Programu ya The Feed the Future imetumia zaidi ya Tsh.Bilioni 8 katika kuwezesha vijana, Mikoa iliyonufaika na Mradi huo ni Iringa na Mbeya kwa upande wa Tanzania Bara, unguja na Pemba kwa Tanzania Visiwani.
Leave a Comment
Your email address will not be published. Required fields are marked with *